NNI IJUMAA HII PALE MBEZI BEACH K.K.K.T
MIMI NA YESU
YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA
7 Apr 2015
4 Apr 2015
TABIA NA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU (MST. 8-11, 13-15)
Katika mistari hii, tunajifunza kuhusu tabia na kazi za Roho Mtakatifu. Ingawa Roho Mtakatifu ana tabia na kazi nyingi zaidi kuliko zile zilizoorodheshwa hapa, hata hivyo, katika mistari hii, tunajifunza tabia na kazi zake za msingi. Zifuatazo ni kazi za Roho Mtakatifu zinazotajwa katika mistari hii:-
- KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA DHAMBI: – Watu wote ambao hawamwamini Yesu, wanafanya dhambi (MST. 9). Watu wengi ingawa hawamwamini Yesu, hujihesabia haki kutokana na amtendo yao kama Farisayo yule katika LUKA 18:9-14. Watu wengi hujihesabia haki na kujiona kwamba hawana dhambi, kwa kuwa wanashika taratibu zote za dini zao, kama walivyofundishwa (MATENDO 26:4-5; WAGALATIA 1:14). Kutokana na msingi huu, Sauli alijihesabia haki na kuona kwamba yeyote ambaye alikuwa hafuati taratibu zote za dini yake, ndiye mwenye dhambi na alifaa hata kuuawa. Aliposikia sauti ya Yesu ikisema, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Alishangaa, maana aliona anatenda haki yote. Tukitoka na kwenda kuwahubiria watu wa jinsi hii ya Farisayo na Sauli, na kutaka waokolewe, bila msaada wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kufanikiwa, kwa sababu wao watajiona kuwa hawana dhambi na kutuona sisi ndiyo tuliopotea kwa sababu hatuko katika dini zao! Mtu ambaye havuti sigara, hanywi pombe, haibi, hafanyi ushirikina, haui au hatukani matusi, mtu wa namna hii ni vigumu kumshawishi kwamba ana dhambi, na kumtaka atubu na kuokolewa, kwa kumfundisha tu kwamba, sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu tangu kuzaliwa (ZABURI 51:5; WARUMI 3:10-12, 23; 1 YOHANA 1:8-10). Sasa basi, ni kazi ya Roho Mtakatifu kumfanya kila mtu wa namna hii, anayejihesabia haki, kushtakiwa na dhamiri yake na kujiona hafai na ni mwenye dhambi (YOHANA 8:3-9). Ndiyo maana, tukitoka kuwahubiri watu na kutegemea ujuzi wetu tu wa maandiko bila msaada wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kupata matokeo makubwa. Hatuna budi wakati wote kuitambua kazi hii ya roho Mtakatifu, na kumkaribisha aambatane pamoja nasi kila tunaposimama kuhubiri au kufundisha ili ashuhudie pamoja nasi (YOHANA 15:26-27). Tukifanya hivi, huduma zetu zitakuwa na mafanikio makubwa. Hatuna budi kupokea uwezo utokao juu, Nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuwe mashahidi wa Yesu wenye uwezo wa kuwaleta wenye dhambi wengi kwa Yesu (LUKA 24:48-49; MATENDO 1:4,8).
- KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA HAKI: – Ni kazi ya Roho Mtakatifu kumhakikishia kila tunayemhubiri kwamba Yesu Kristo pekee ndiye mwenye haki na tunahesabiwa haki kwa kumwamini Yeye tu (1 YOHANA 2:1). Roho Mtakatifu akitenda kazi hii humfanya mtu akiri kwamba Yesu ndiye mwenye haki, kama ilivyokuwa kwa akida katika LUKA 23:47. Vivyo hivyo, Roho Mtakatifu huwahakikishia watu tunaowahubiria kwamba maneno yale tunayoyasema ndiyo ya haki, na kweli., kuliko yale waliyojifunza katika dini zao. Tukiwa na Roho Mtakatifu, hatuna haja ya kutumia Misahafu ya dini nyingine kuwahakikishia watu tunavyowahubiri. Kufanya hivyo, ni ubatili, maana ni kuvithibitisha vitabu hivyo kwamba vina ukweli, na hilo haliwezi kuleta matokeo.
- KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA HUKUMU: – Watu wengi wenye dhambi, hawaamini kwamba kuna hukumu ya kutupwa motoni baada ya kufa, na kuona kama ni mbinu za kuwaanya waache starehe za dunia. Watu wengi pia hawaamini kwamba wanaweza kusamehewa dhambi zao kabisa na kufutiwa hukumu, na hudhani kwamba hata wafanyeje kama wameandikiwa motoni basi. Kazi ya roho Mtakatifu, ni kumhakikishia mtu tunayemhubiria kwamba ni kweli kuna hukumu baada ya kufa na Mhukumu wa Ulimwengu huu ni Yesu. Vilevile humhakikishia kwamba Mkuu wa Ulimwengu Shetani, yeye amekwisha kuhukumiwa kutupwa katika moto wa milele, na hana nafasi ya kusamehewa, laki8ni sisi tuna nafasi ya kufutiwa hukumu tukimwamini Yesu (WAEBRANIA 9:27; MATHAYO 25:41; YOHANA 3:18, 36). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu ndipo mtu anapoweza kusema kama mhalifu msalabani katika LUKA 23:39-42.
- KUWAONGOZA WATU NA KUWATIA KWENYE KWELI YOTE: – Roho Mtakatifu, huwaongoza watu na kuwaonyesha njia ya kweli. Anaweza hata kusema na watu kwa njia ya ndoto kama mkewe Pilato (MATHAYO 27:19), na kuwaelekeza waende kusali Kanisa fulani, waende katika mkutano fulani wa Injili n.k. Roho Mtakatifu huwapeleka watu kwenye kweli. Ndiyo maana tukiwa hatuhubiri kweli katika makanisa yetu, tutaona watu wengi wanachomoka na kuhama wakiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye kweli yote, na kwa kukosa ufahamu, tutalalamika kwemba watu wetu WANAIBIWA! Roho Mtakatifu hawaibi! Ni watu wake! Roho Mtakatifu huwaongoza watu kwa wingu na moto (HESABU 9:15-23). Tabia za Roho Mtakatifu, ni pamoja na hizi zifuatazo tunazojifunza katika mistari hii:
- HANENI KWA SHAURI LAKE MWENYEWE: – Maneno ya Roho Mtakatifu SIKU ZOTE hufanana na maneno ya Yesu, hayatofautiani kamwe maana Roho Mtakatifu hutwaa katika yaliyo ya Yesu na kutupasha habari (MST. 13-15). Yeye ni roho wa kweli, na Yesu ndiye Kweli, hivyo ni sawa pia kusema Yeye ni Roho wa Yesu (MATENDO 16:7). Roho Mtakatifu, hushuhudia pamoja na Baba na Mwana (1 YOHANA 5:8). Hivyo mtu akisema ameongozwa na Roho Mtakatifu kumwacha mkewe na kumwoa mke mwingine, ni dhahiri kwamba huyo siyo Roho Mtakatifu, maana Yesu alisema amwachaye mkewe na kumwo mwingine azini, na Baba anachukia kuachana (LUKA 16:18; MALAKI 2:15-16). Ujumbe au unabii wowote unaodaiwa kwamba unatokana na Roho Mtakatifu, kwa msingi huu, lazima tuupime kwa Neno la Mungu.
- NI ROHO WA KWELI: – Hasemi uongo, hivyo ujumbe unaotokana na Roho Mtakatifu unaotupasha habari ya mambo yajayo, hauna budi kutimia. Hata hivyo, hata ukitimia, lakini unatutoa mbali na kweli ya Neno la Mungu, tujue pia siyo wa Roho Mtakatifu (KUMBUKUMBU 13:1-4). Inatupasa kuwa waangalifu nyakati za leo kuweka mawazo yetu katika unabii, Roho hutumia njia hii leo mara chache sana, maana anasema nasi leo katika Neno la Mwana wa Mungu Yesu (WAEBRANIA 1:1-2). Katika Matendo ya Mitume,
tunaona jumbe chache sana za Roho Mtakatifu kwa miaka mingi!
21 Nov 2014
sOMO:
MAMBO YATAKAYOLIFANYA JINA LA YESU LIKUPE MATOKEO
Leo nimeamka nikiwa na mzigo na kiu ya kukupa siri hizi zitakazo kusaidia kuwa na ubora na ufanisi katika matumizi ya Jina kuu la Yesu.
Maana kwa Wakristo wengi limekuwa ni jina lisilotoa matokeo na kufanya makubwa kama lilivyofanya nyakati za Mitume wa Yesu na kanisa la kwanza. Naomba ujitahidi kulipitia somo hili kwa umakini na moyo uliofunguka na hakika utapokea kiwango kipya cha ufunuo na upako uliomo ndani ya jina hili kuu la Yesu.
Nakukaribisha, katika jina la Yesu.
Mstari wa kusimamia:
"Kwa maana kila atakayeliitia jina la BWANA ataokolewa" (Warumi 10:13).
Utangulizi:
Matatizo mengi tuliyonayo yametokana na KUFUMBA MDOMO na kuacha KULITUMIA JINA LA YESU KWA IMANI.
Wengi wanalitumia JINA LA YESU kama kibwagizo cha maombi, na kwa namna hiyo haliwezi kutoa matokeo.
Unapotaka jina la Yesu likupe matokeo lazima ujue na kufanyia kazi mambo yafuatayo:
1. Ni jina TULILOPEWA KISHERIA NA MUNGU kutawala na kumilki na kufunga na kufungua chochote duniani kama Ufunguo wa Ufalme wa mbinguni:
"Kwa maana hakuna JINA JINGINE TULILOPEWA litupasalo kuokolewa kwalo" (Mdo 4:12).
Biblia inasema hili JINA LA YESU tumepewa liwe la kwetu kisheria.
Ni JINA TULILOPEWA si "jina tuliloazimwa" kwa muda.
Ukielewa na kuamini kwamba JINA LA YESU NI MALI YAKO pamoja na mamlaka na nguvu iliyomo ndani yake, Hakika Utaanza kulitumia bila hofu na mashaka wala hautalisema kama kibwagizo cha maombi, na litakupa matokeo na miujiza isiyokuwa ya kawaida.
2. Elewa kwamba IMANI YAKO KUHUSU JINA LA YESU inapaswa kuwa sawa na IMANI YAKO KWA YESU MWENYEWE.
Unajua kuna watu WANAMWAMINI MNO YESU, na wanaamini kama angekuwepo "Live" kimwili, angeweza kutatua na kukomesha kila msiba wao.
Lakini watu hawa HAWANA IMANI YA KIWANGO HICHOHICHO kwa JINA LA YESU.
Zingatia hili:
Yesu kama "mwili" ameketi mkono wa kuume mbinguni anatuombea sasa (Waebrania 7:25, 1Yoh 2:1-2, Warumi 8:33-34).
Yesu kama "mwili" yuko mbinguni akituandalia makao (Yohana 14:1-3).
Hivyo Yesu akiwa kama "mwili" hawezi kutokea na kukusaidia.
Yesu yuko pamoja nasi siku zote hata ukamilifu wa dahari kupitia Roho wake mtakatifu ambaye ametupa kama arabuni (guarantee) hata siku ya unyakuo na kupitia JINA LAKE.
Ili Yesu atokee katika ulimwengu wa roho na kukifanya ukitakacho itakubidi uliamini jina lake kwa kiwango kilekile unachomwamini Yeye kama angekuwepo live!
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu, ndio wale WALIAMINIO JINA LAKE" (Yoh 1:2).
Mstari huu wa Biblia unaongelea na kutuonyesha "IMANI KATIKA JINA LA YESU" ambayo ni kuliamini jina lake kwa kiwango kilekile ambacho unakiamini kama Yesu angekuwepo mzimamzima!
Ukisoma Matendo 3:16, utagundua kwamba KILICHOMFANYA KIWETE ATEMBEE NI IMANI KATIKA JINA LA YESU.
Utakapoanza kuambatanisha imani yako yote KATIKA JINA LA YESU kwa kiwango kilekile ambacho ungemwamini Yesu kama ungekutana naye live, hakika miujiza mikubwa itaanza kutokea maishani mwako na kupitia maneno na mikono yako!
"Nimewaandikia ninyi mambo haya ili mjue ya kwamba mnao Uzima wa milele ninyi MNAOLIAMINI JINA LA MWANA WA MUNGU" (1Yoh 5:13).
Kumbuka uzima wa milele ni nuru iliyomo ndani ya mwamini ambayo inapong'aa gizani, giza haliiwezi na halitakuja kuiweza milele (Yoh 1:4-5).
Na huu uzima wa milele unaopindua giza uko mikononi na ndani yao WANAOLIAMINI JINA LA MWANA WA MUNGU, JINA LA YESU!
3. Elewa kwamba MAMLAKA YOTE ALIYONAYO YESU imefungwa ndani ya JINA LAKE.
Yesu alipofufuka na kuwatokea wanafunzi wake, aliwaambia AMEIPINDUA SERIKALI YA SHETANI.
Aliwaambia ANAYO MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI (Mathayo 28:18).
Lakini ukisoma Biblia yako vizuri utagundua hii mamlaka yake IMEWEKEZWA KATIKA JINA LAKE.
Wafilipi 2:5-11 inatuambia kwamba:
Yesu alipokubali kutii na kujinyenyekeza hata mauti ya msalaba na kutimiza kusudi la babaye alilompa, ndipo Mungu alimkirimia JINA LIPITALO MAJINA YOTE ili kila kitu cha MBINGUNI, DUNIANI NA KUZIMU kitii na kujisalimisha kwa Yesu Kristo (kipige goti) na kikiri kuwa YESU KRISTO NI BWANA kwa utukufu wa Mungu Baba.
Hii ni mamlaka na mamlaka hii imewekwa ndani ya JINA LA YESU.
Ukielewa kuwa mamlaka yote aliyonayo Yesu imewekwa katika jina lake kama yasemavyo maandiko, itakusaidia kupandisha Imani yako na thamani yako katika jina la Yesu na litaanza kukupa matokeo kila ukilitumia.
Jina la Yesu linafanya kazi kwa wenye maarifa na siri hii.
4. Elewa kwamba jina la Yesu ni kitu halisi (ni roho) kwenye ulimwengu wa roho.
Usipoelewa kwamba jina hili la Yesu ni KITU HALISI (ROHO) katika ulimwengu wa roho, hautaweza kulitumia kufanya mambo makubwa rohoni.
Daudi alijua siri hii, alijua ya kuwa JINA LA BWANA ni kitu halisi katika ulimwengu wa roho kiasi kwamba wakati Goliati anakuja na Panga, fumo na mkuki, Yeye (Daudi) naye alichukua silaha halisi isiyoonekana kwa macho ila inayotajwa kwa mdomo, JINA LA BWANA na akapata ushindi wa kishindo dhidi ya Goliati na kuua MAKUMI ELFU YA WAFILISTI.
Kasome 1Samweli 17 utaona jambo hili kwa uwazi.
"JINA LA BWANA NI NGOME IMARA wenye haki hulikimbilia wakawa salama" (Mith 18:10).
Kwa leo niishie hapa,
Mwl Dickson Cornel Kabigumila
20 Nov 2014
Maana ya wokovu
Wokovu ni kazi ya Mungu kwa ajili yetu (1Tim 2:4; 2Tim 1:9-10). Sisi hatuwezi kujikomboa, lakini Mungu ana nguvu kuliko shetani na mabaya yote, naye anatuhurumia sisi maskini (Kol 1:13-14). Alifanya nini ili kutuokoa? Ndiyo historia ya wokovu. Wapo walioiandika katika Biblia ili tusadiki na kuishi upya (1Pet 1:10-12). Humo mtu hatazamwi kama nafsi ya peke yake tu, bali zaidi kama mtu wa taifa lake; hivyo Mungu anatangazwa kuwa hashughulikii wokovu wa mtu binafsi tu, bali wa mataifa mazima pia, kuanzia lile la Israeli. Aliyowatendea wao ni hasa kuwatoa utumwani Misri, kuwapa agano na masharti yake li awafanye taifa huru katika nchi bora. Waisraeli walijenga imani yao juu ya hayo mang’amuzi ya msingi ya wokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, halafu wakajikumbusha kwamba alikuwa ameshawaahidia mababu wao baraka kama hizo. Hatimaye tu walitafakari juu ya asili ya watu na ya ulimwengu, wakaelewa kuwa Mungu aliweza kuwaokoa kwa sababu ndiye aliyeumba vyote: hakuna wa kushindana naye na wa kuzuia mpango wake kwa ajili ya watu. Kwa Wakristo tukio kuu lililo msingi wa imani ni ufufuko wa Yesu, aliyetoka kaburini mzima na mtukufu, wa kwanza kati ya umati, akaingia katika nchi ya walio hai kweli.15 Nov 2014
USHINDI KATIKA UJANA
Kijana ni nani?
Kijana ni mtu wa kike au wa kiume mwenye umri kati ya miaka 15 na 45.
Kijana ni mtu wa kike au wa kiume mwenye umri kati ya miaka 15 na 45.
Biblia inasema nini juu ya kijana?
Biblia imenena mambo mengi juu ya kijana, na baadhi ya hayo ni kuwa fahari ya kijana ipo katika nguvu zake (Mithali 20:29). Kijana ana nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa ndani yake na kisha amemshinda shetani(1Yohana 2:14b).
Biblia imenena mambo mengi juu ya kijana, na baadhi ya hayo ni kuwa fahari ya kijana ipo katika nguvu zake (Mithali 20:29). Kijana ana nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa ndani yake na kisha amemshinda shetani(1Yohana 2:14b).
Yohana anawaandikia vijana akisema wana nguvu nyingi, pili neno la Mungu linakaa ndani yao na kisha wamemshinda shetani. Nguvu yaweza kuwa ya kiroho au ya kimwili, maana zote ni za muhimu na mara nyingine hutegemeana katika utendaji.
Nguvu moja ikikosekana hujitokeza upungufu unaoweza kupelekea uharibifu kama vile mtu kurudi nyuma kwa sababu ya majaribu. Nguvu ya kimwili ya mtu wa Mungu ikitumika kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu, yaweza kupelekea mtu kuwa na nguvu ya kiroho iletayo ushindi juu ya hila na mitego ya yule mwovu.Hapa ina maana kuwa, kwa mtu wa Mungu ukiwa na nguvu ya kimwili na unaongozwa na Roho wa Mungu utamtumikia Mungu pasipo ulegevu, tofauti na mzee ambaye anaweza kuhitaji kufanya jambo lakini nguvu ya kwenda kufanya hana, hilo nalo Mhubiri aliliona na kumhamasisha kijana kutumika akiwa bado anazo nguvu. Mhubiri12:1 ”Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…“ Yohana anawaandikia vijana akionyesha sifa za aina ya vijana aliokuwa akiwalenga. Anatazamia kwamba kijana akiitumia nguvu hiyo kama ilivyokusudiwa na Mungu, na kulisoma neno, kuomba kwa bidii zake zote, matokeo yake atakuwa na hazina tele ya neno ndani mwake, na kisha atamshinda shetani, maana anazo nguvu za kiroho na za kimwili. Kijana wa aina hii hana hofu maana hata shetani akija kwa sura gani au akitumia mazingira gani, haogopi maana silaha alizo nazo (Neno) ni tishio kwa adui. Mungu anawatafuta vijana kama hao wabebao silaha hiyo ya Bwana , nyakati zote, kila mahali na kwa bidii. ”..Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu“(I Yohana 2:14b).
Nguvu moja ikikosekana hujitokeza upungufu unaoweza kupelekea uharibifu kama vile mtu kurudi nyuma kwa sababu ya majaribu. Nguvu ya kimwili ya mtu wa Mungu ikitumika kwa mujibu wa uongozi wa Roho Mtakatifu, yaweza kupelekea mtu kuwa na nguvu ya kiroho iletayo ushindi juu ya hila na mitego ya yule mwovu.Hapa ina maana kuwa, kwa mtu wa Mungu ukiwa na nguvu ya kimwili na unaongozwa na Roho wa Mungu utamtumikia Mungu pasipo ulegevu, tofauti na mzee ambaye anaweza kuhitaji kufanya jambo lakini nguvu ya kwenda kufanya hana, hilo nalo Mhubiri aliliona na kumhamasisha kijana kutumika akiwa bado anazo nguvu. Mhubiri12:1 ”Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…“ Yohana anawaandikia vijana akionyesha sifa za aina ya vijana aliokuwa akiwalenga. Anatazamia kwamba kijana akiitumia nguvu hiyo kama ilivyokusudiwa na Mungu, na kulisoma neno, kuomba kwa bidii zake zote, matokeo yake atakuwa na hazina tele ya neno ndani mwake, na kisha atamshinda shetani, maana anazo nguvu za kiroho na za kimwili. Kijana wa aina hii hana hofu maana hata shetani akija kwa sura gani au akitumia mazingira gani, haogopi maana silaha alizo nazo (Neno) ni tishio kwa adui. Mungu anawatafuta vijana kama hao wabebao silaha hiyo ya Bwana , nyakati zote, kila mahali na kwa bidii. ”..Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu“(I Yohana 2:14b).
Biblia inasema kijana akilitii Neno la Mungu na kulifuata litasafisha njia yake. Litamkamilisha kwa kiwango anachotaka Mungu, kwa makusudi ya Mungu na kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ili kijana aweze kuishi maisha matakatifu, yenye ushindi tele na yanayomtukuza Mungu yampasa kuisafisha njia yake kwa kutii, akilifuata neno la Mungu. Zab.119.9 ”Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.“
Kijana, kufanikiwa kuisafisha njia yako kutategemeana na wewe mwenyewe utakavyotumia nguvu zako. Yakupasa kuelekeza nguvu zako katika maombi, kujisomea Neno la Mungu, hii ni pamoja na kulitafakari na kulitendea kazi. Kwa kufanya hivyo utapata nafasi nzuri ya kumsikiliza Mungu na kujua ni nini mpango na makusudi yake kwako. Kijana hupaswi kulala usingizi tangu jioni hadi asubuhi na tangu January hadi Desemba, huo ni msiba wa kutosha kwa kijana maana Biblia inasema mtu wa aina hiyo atapata umaskini wa kumtosha. Si vema kijana kuzagaa, ukikutwa na adui ukiwa umezagaa atakutumikisha katika matakwa yake. Ni muhimu sana kijana kuwa na mikakati na kuiombea ili kupata uongozi wa Roho Mtakatifu. Mungu anajali sana kijana kuwa na mkakati. Mfano mzuri ni namna alivyomwandaa Yoshua kushika nafasi ya Musa. Awali ya yote alimhakikishia uwepo wake pamoja na kijana huyo, na akamwahidi kutomwacha wala kumpungukia kabisa: ”Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako…sitakupungukia wala sitakuacha.“ (Yoshua 1. 5).
Hapa Mungu anamhakikishia Yoshua kuwa, hata kutokee tatizo kubwa kiasi gani, hata vitisho viwe vikubwa namna gani, hata ainuke nani, asingeweza kuzuia wala kukwamisha kusudi la Mungu katika huduma aliyokuwa anakabidhiwa na Mungu, ya kuwafikisha Waisraeli nchi ya Kanaani. Hali kadhalika wewe kijana, yumkini bado unawategemea wazazi au ndugu, lakini kwakuwa umeokoka labda wamekutenga, hawataki kukupa huduma, hata masomoni unatishiwa kufukuzwa kwasababu huna karo; yumkini umeoa au umeolewa na huyo mume au mkeo anakutesa kwa ajili ya wokovu; kazini unanyanyaswa na mkubwa wako wa kazi au wafanyakazi wenzio, halikadhalika kwenye biashara zako wanakutesa kwa njia mbalimbali. Katika hali yoyote ile, jambo la muhimu uwe na uhakika kwamba Mungu yupo pamoja na wewe na kwamba hatakuacha wala hatakupungukia. Hivyo usikate tamaa, azimia kutomwacha Mungu kabisa, simama katika haki na ahadi za Mungu, utaona ushindi mkubwa.
Baada ya Mungu kutoa uhakika juu ya uwepo wake kwa kijana huyo Yoshua, alimpa mikakati ya namna atakavyoweza kufikia lengo ambalo lilikuwa kuwafikisha Waisraeli katika nchi ya ahadi, Kanaani. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi….
Mungu hapendezwi na uvivu, alitaka Yoshua awe hodari tu na ushujaa mwingi na siyo mtu wa kujihurumia hurumia bali awe mwepesi wa kwenda anakotakiwa, kutekeleza majukumu ambayo Mungu angempa inavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa, na pasipo hofu. Huo ndiyo ushujaa.
Mungu hapendezwi na uvivu, alitaka Yoshua awe hodari tu na ushujaa mwingi na siyo mtu wa kujihurumia hurumia bali awe mwepesi wa kwenda anakotakiwa, kutekeleza majukumu ambayo Mungu angempa inavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa, na pasipo hofu. Huo ndiyo ushujaa.
2. ...uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume au wa kushoto.(Yosh. 1.7).
Mungu anamwambia Yoshua, aangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuwa ameamriwa na Musa mtumishi wake Mungu. Swala kuu hapa ni utii wa neno la Mungu. Kwamba kijana hatarajiwi kuwa msikilizaji tu wa Neno la Mungu na kuendelea na maisha ya kidunia. Kijana anahitajika kuwa msikiaji na mtendaji/mtekelezaji wa maagizo ya Mungu ndani ya Neno.
Mungu anasisitiza katika mstari wa nane kuhusu kutafakari Neno. Mungu alimtaka Yoshua, kuhakikisha siku zote za maisha yake anafanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha yake. Alimtaka akiwaza awaze (atafakari) Neno mchana na usiku, maongezi yake yawe na msingi katika Neno. Kuhusu kutendea kazi Neno, Mungu alimwambia Yoshua aangalie kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo (ndani ya torati/Neno.
”Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo…."(Yoshua 1:8).
Kwa maana hiyo, iwe usiku iwe mchana kijana saa zote unatakiwa kutafakari neno la Mungu siyo kuwaza shida, taabu na masumbufu ya dunia hii. Kulitafakari Neno huja baada ya kulisoma, Daudi alisema: ”Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi“ (Zab. 119.11).
Alilisoma na kisha akalihifadhi moyoni. Neno hilo katika hazina ya moyoni, likawa mshauri, mwongozo na faraja wakati wa majaribu, mapito au mateso. Na kwa kulitamka likafanyika fimbo ya kumwangamiza adui, na kufungua milango ya baraka iliyofungwa na adui na pia likatumika hata kubadilisha mazingira kama Ezekia alivyotamka uhai kwa mifupa, ikainuka ikiwa hai na kuwa kikundi kikubwa cha watu.
Ili uwe na maisha yenye mwelekeo wa ki-Mungu na ya mfano, epuka kabisa kuwaza mambo mapotofu, epuka mazungumzo mafu yasiyo na uhai wa ki-Mungu maana yatakuharibu wewe pamoja na wakusikilizao, pia matendo yoyote yaliyo kinyume na Neno la Mungu epukana nayo. Mungu alijua kuwa kijana huyu Yoshua asiposisitiziwa na Mungu mwenyewe, asipoishi kwa Neno ambalo ndiyo lishe bora ya roho yake, angeharibikiwa, na hapo kusudi la Mungu la ukombozi wa wana wa Israel lingeyumba. Hali kadhalika wewe usipoishi kwa kulitii Neno na kufanya kama linavyokuagiza, adui atayumbisha mpango wa Mungu katika maisha yako, matokeo yake ni kuchanganyikiwa, kukata tamaa na hata kufa kabisa kiroho. Lakini ukisimama pasipo kujali mazingira yanayokuzunguuka, Mungu anao mpango mzuri sana na maisha yako na ndiyo maana amekuokoa (amekuita). Yumkini wewe ndiye wa kwanza kumpa Yesu maisha yako katika familia au ukoo wako. Mungu anategemea kukutumia wewe kulifikisha kundi hilo nchi ya ahadi kama alivyomtumia Yoshua. Zoezi hilo litafanikiwa iwapo utakuwa hodari tu na mwenye ushujaa mwingi, na kutenda sawasawa na Neno kama linavyoletwa kwako na Roho Mtakatifu mwenyewe kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujumbe huu unaousoma sasa.MUNGU akubariki sana
10 Nov 2014
Kanisa halipaswi kuazima mitindo ya
kiganga kuendesha huduma za maombezi. Mitindo ya kiganga ni pamoja na matumizi
ya misamiati inayotumika kwenye anga za wapunga pepo, pamoja na kutumia
Askofu
Sylvester Gamanywa.
|
uzoefu wa kiganga/kichawi mtu aliuokuwa
nao kwenye ulimwengu wa giza na kuuleta katika huduma za kikanisa.
Hatari ya kuendekeza hii hali ni
kuanguka kwenye mitego wa Ibilisi wa kujaribu kudhoofisha utendaji halisi wa
nguvu za Roho Mtakatifu. Kumbuka Yule aliyekuwa Mchawi alivyotaka kununua
uwezo/karama ya kuwekea watu ujazo wa Roho Mtakatifu ili autumie kwenye uzoefu
wa kichawi aliokuwa kiufanya na kushangaza wengi huko Samaria.
Kama sio Petro kupitia karama ya
maarifa kumgundua hila zake si ajabu hata kama asingepokea fedha lakini angemkubalia
kuifanya huduma ya kuombea watu Roho Mtakatifu na badala ya watu kujawa na Roho
Mtakatifu wangejazwa “roho mtakafujo”!
Kwa hivi sasa, sio siri kwamba,
tayari wako watu waliojiingiza katika huduma za maombezi kwa madai ya
kuwafungua watu katika vifungo vya majini lakini miitndo inayotumika katika
huduma hizo inaonesha dalili zote za “wapunga pepo” wanaotumia uzoefu wa
kiganga/kichawi. Utawatambuaje? Ziko dalili za waziwazi kama Yesu alivyotabiri:
“Mtawatambua kwa matunda yao.”:
Wanajiita watumishi wa Mungu lakini
tabia na mienendo yao haina maadili ya utumishi wa Kristo. Wamejaa mizaha na
utovu wa nidhamu usioambatana na utendaji wa huduma za kweli zinazomwakilisha
Kristo katika utumishi.
Kipaumbele sio kuwafundisha watu
kumjia na kumjua Kristo na kuishi maisha ya utakatifu wa kweli. Wanachojali ni
kuteneza wafuasi wengi wataoendelea kuwa na “imani tegemezi” kwao; badala ya
kuwafundisha watu kumtegemea Kristo ambaye kimsingi ndiye mwenye mamlaka kamili
ya kuwafungua na kuwaweka watu huru mbali na vifungo vya pepo wachafu.
Mara nyingi kipambele katika huduma
ni kukusanya fedha kwa visingizio vya “jumbe zi kinabii” lakini zenye
kuambatana na malipo kama kigezo cha kufunguliwa kwa wagonjwa na wenye pepo.
Hii ndiyo ile ya Yule Simoni mchawi akiyeingiza suala la “kununua karama ya
Mungu kwa mali” ili apate kuifanyia biashara katika maombezi
Kanisa
halipaswi kupokea na kufanyia kazi
ushauri
wa mapepo katika maombezi
Hili ni onyo kwa watumishi wa kweli
wanaofanya huduma za maombezi, lakini pasipo kujua au kukusudia, wamejikuta
wametumbukia katika mtego wa kutegemea taarifa zinazotolewa na mapepo
yaliyowapagaa watu zinazodai sababu za kuwapagaa na nini kifanyike ili
wawaachie waliowapagaa.
Watumishi wa kweli wa Kristo,
hawapaswi, kwa namna yoyote ile; kupokea na kufanyia kazi ushauri wa mapepo
kama ndio mtindo na njia ya watu waliopagawa wapate kufunguliwa!
Kwa kusema hivi sina maana kwamba
pasiwepo kabisa mawasiliano na pepo wanapowapagaa watu. Ninachomaanisha ni
kwamba wakati wa “mawasiliano na pepo”, ajenda kuu iwe ni “kuyakemea na
kuyaamuru yatoke kwa mamlaka ya Kristo pasipo kutafuta kuwa na muafaka wa
masharti ya mapepo”!
Uchunguzi na uzoefu nilioupata
katika utumishi huu wa huduma za maombezi, ninao ushahidi wa kutosha
kuthibitsha kwamba, sio wote wanaopagawa na pepo wakati wa maombezi hufunguliwa
mara moja. Wengine huchukua muda kutokana na mfumo wa maisha wanayoishi,
ufahamu duni wa Neno la Mungu, na utayari wa kujitoa kikamilifu kuishi maisha
ya utakatifu kama yasemavyo maandiko.
Kwa hiyo mapepo kupiga kelele na
kuangusha watu chini wakati wa maombezi; kisichukuliwe kuwa kigezo pekee kwa
wahusika wanafunguliwa. Kufunguliwa katika pepo kwa walio wengi ni mchakato
ambapo wahusika wanatakiwa kutoa ushirikiano makini ikiwa ni pamoja na kuhimizwa
kupokea wokovu wa Yesu Kristo, na utayari wa kupitia mafundisho makini ya Neno
la Mungu na, utayari wa kubadilika kitabia na mwenendo kama njia ya
kufunguliwa kikamilifu.
Mungu
alikwisha kutoa mamlaka
ya
kudhibiti uchawi kanisani
Ni wakati wa kanisa sasa kurejea
kwenye ufunuo wa kanisa la kwanza na kuwa na mamlaka ile ambayo Kristo
aliwakabidhi mitume wake kama ilivyoandikwa:
“Akawaita wale Thenashara, akawapa
uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. (LK. 9:1)"
Katika makala yaliyopita tulifunza
kupitia maandiko haya kuhusu neno hili “Uwezo” kwa kiyunani linaitwa “Dunamis”
lenye kumaanisha “nguvu ya kutenda miujiza ya uumbaji, au kuharibu nguvu za
pepo wabaya”! Kwa hiyo, Yesu Kristo alipowapa wanafunzi wake “uwezo na mamlaka”
juu ya pepo wote, maana yake aliwapa nguvu za kufukuza au kutoa pepo wabaya
watoke ndani ya watu wengine bila mjadala!
Pia tuliwahi kujifunza kwamba Bwana
Yesu alipoagana na wanafunzi wake, aliwaahidi kupokea hii nguvu ya “dunamis”
mara tu Roho Mtakatifu atakapowashukia.
“Lakini mtapokea nguvu (dunamis) akiisha kuwajilia juu yenu Roho
Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu kuanzia Yerusalemu, uyahudi wote,
Samaria hata mwisho wa nchi.” (Mdo.1:8)
Mwisho kabisa, tunauoa utendaji wa
mamlaka ya kupambana na kuvunja shughuli za uganga/uchawi kila mahali ambapo
Injili ya Kristo ilipohubiriwa:
“Na watu wengi katika wale
waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya
watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha
hamsini elfu. Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa
nguvu.” (MDO 19:19, 20)
Maandiko haya yanashuhudia jinsi
kanisa la kwanza lilivyotamba dhidi ya nguvu za uchawi na kuleta maelfu katika
ufalme wa Mungu. Huu ndio uamsho unaohitajika makanisa wa kuendesha huduma za
maombezi yenye mamlaka halisi ya nguvu za Roho Mtakatifu na kuonesha matokeo ya
kufunguliwa kikamilifu kwa wote wanaomjia Kristo.
Haifai kabisa kanisa kuendelea
kuongozwa na ushauri wa mapepo ambao huwajengea hofu waamini badala ya ujasiri
wa kutoa pepo. Kumbuku Yesu Alisema “ishara hizi zitafuatana na hao waaminio
kwa jina langu watatoa pepo” na sio “Hofu ya uchawi itafuatana na hao waaminio
nao watapunga pepo”!?
Mwisho
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)